Sunday, October 10, 2010

PROFESA MWANDOSYA ZIARANI INDIA.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya yuko india wiki hii kwa ziara fupi kwa mwaliko wa Dr Rajendra Pachauri (pichani shoto) Mkurugenzi mkuu wa Tata Energy and Resource Institute (TERI) na Mwenyekiti wa Jopo la kimataifa la Wataalam wa mabadiliko ya Tabiachi (International Panel on climate Change IPCC) DrRajendra Pachauri ni mshindi wa tuzo ya Nobel ya Amani ya mwaka 2009 ambayo akiwakilisha IPCC alipokea tuzo pamoja na Bw. Al Gore Makamu wa Rais Msitaafu wa Marekani.Profesa Mwandosya na Dr Pachauri wamezungumzia maswala ya maji, nishati, mazingira, maliasili,ushiriano na maendeleo endelevu. Profesa Mwandosya ametembelea Chuo Kikuu cha TERI na Kituo Kikuu cha utafiti cha TERI.Profesa Mwandosya akimkabidhi zawadi Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha TERI, Profesa Bhavit Bakishi. Profesa na Mama Mwandosya wakipata maelezo ya utafiti katika matumizi ya mionzi ya jua kwa umeme wa nyumbani katika maabara ya chuo kikuu cha TERI
Profess akipata maelezo kuhusu biotechnologia katika kituo cha utafiti cha TERI nje kidogo ya new Delhi Profesa Mwandosya alipata nafasi kuwatembelea wa Tanzania waliolazwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi. Hapa anasalimiana na Meja Generali (Msitaafu) Silas Mayunga Profesa Mwandosya akiwa na badhi ya wafanyakazi wa ubalozi, new delhi, India. Toka shoto ni Mama Kiondo, Profesa, Nd. Mwamanenge na Mama Amina



No comments:

Post a Comment