Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa mkutano wa kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliokuwa ukijadili ajenda ya upokonyaji wa silaha na usalama wa Kimataifa, ambapo pamoja na mambo mengine aliushauri Umoja wa Mataifa kutumia teknolojia ya panya wanaozalishwa na kupatiwa mafunzo ya kugundua mabomu ya ardhini. Mradi huo unafanyika nchini Tanzania ukizishirikisha Taasisi ya Ubelgiji ijulikanayo kama APOPO, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ)
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
Tanzania imeushauri Umoja wa Mataifa kuangalia uwezekano wa kutumia panya wenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini.
Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue wakati alipokuwa akichangia majadiliano ya Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia upokonyaji wa silaha na usalama wa kimataifa.
Akiunadi mradi wa kutegua mabomu ya ardhini kwa kutumia panya unaotekelezwa na asadi isiyo ya kiserikali ya Ubelgiji ijulikanayo kama APOPO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, katika kuwafundisha na kutumia panya kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini.
Anasema “ Teknolojia hii imekwisha kutambuliwa ndani ya Umoja wa Mataifa na baadhi ya nchi zimeshaitumia kutegua mabomu kwa mafanikio makubwa. Tunaukaribisha Umoja wa Mataifa, Jumuia ya Kimataifa na nchi wanachama kuunga mkono na kuutumia utaalamu huu ambao ni rahisi, salama na wagharama nafuu”.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akasisitiza kwa kusema kwa miaka mingi na baada ya kumalizika kwa vita, watu wengi wasio na hatia katika bara la Afrika na kwingineko wameendelea kupoteza maisha na viungo vya miili yao kunakosababishwa na milipuko ya mabomu ya ardhini.
Akahimiza kwa kusema ikiwa matumizi ya utaalamu huo wa kutumia panya yataongezeka basi maisha ya watu wengi yataokolewa.
Akizungumzia kuhusu uzagaaji na biashara haramu ya silaha ndogo na nyepesi. Balozi Sefue ameueleza mkutano huo kwamba silaha hizo zimekuwa chanzo na kichocheo cha migogoro na uhalifu mkubwa kiasi cha kutishia kudumaza maendeleo ya nchi nyingi duniani, zikiwamo za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Akasisitiza kuwa hatua za Umoja wa Mataifa za kuny’angaya , kudhibiti uzagaaji na biashara haramu ya silaha hizo ni vema ukafanyika sambamba na upokonyaji na udhibiti wa risasi na baruti.
Kuhusu hali tete ya Somalia, Balozi sefue ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Kimataifa kuongeza jitihada za kutafuta suluhu ya migogoro ndani ya Somalia. Pamoja na kuvipokonya silaha vikundi vinavyozorotesha amani na usalama na kupinga juhudi za serikali ya mpito ya Somalia.
Mijadala mingine katika mkutano wa Kamati hiyo ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa itahusu,upunguzaji na udhibiti wa usambaaji wa silaha za nyuklia, silaha nyingine za maangamizi ya halaiki hususan za Kemikali na Baiolojia na udhibiti wa silaha zinazoweza kutumika kwenye anga.
Halikadhalika Kamati hiyo ambayo huzihusisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, pia itajadili hatua nyinginezo za upokonyaji silaha na usalama wa kimataifa, jitihada za upokonyaji wa silaha kikanda na usalama na mjadala wa vyombo vya Umoja wa Mataifa vinavyoshughulikia upokonyaji silaha.

No comments:
Post a Comment