Thursday, October 21, 2010

MWISHO ALIVYOPOKELEWA DAR!


Mwisho Mwampamba akipokea shada la maua kutoka kwa ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jioni akitokea Afrika kusini kwa ndege ya shirika la ndege la SAA ambako alishiriki shindano la BigBrother Africa na kushika nafasi ya tatu huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akijinyakulia kitita cha Dola laki mbili za Kimarekani.
Leo Mwisho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Bigbrother na washiriki wenzake na keshokutwa atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika picha kushoto ni baba yake mzee Mwampamba.
Mwisho Mwampamba akisindikizwa na ndugu zake pamoja na walinzi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jioni ya leo akitokea nchini Afrika Kusini alikoshiriki katika shindano la BigBrother Africa Allstars na kushika nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment