Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa ufafanuzi wa mwamko wake wa kuwa 'Shujaa wa wanawake wenye Fistula' katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika CCBRT leo. Pamoja naye ni Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT Erwin Telemans na Mkurugenzi wa Huduma ya Jamii CCBRT, Brenda Msangi.
===============================
KAMA MWANAMUZIKI WA TANZANIA, NASHUKURU KUWA JAMII YA WATANZANIA WENZANGU WANAPOKEA VIZURI KAZI YANGU YA SANAA YA MUZIKI.
KWA JINSI HIYO BASI……, NA MIMI NINALO JUKUMU LA KURUDI KWA JAMII YANGU NA KUSHIRIKIANA NAO KATIKA HARAKATI ZA KUJIKWAMUA KUTOKA KATIKA MATATIZO MBALIMBALI KAMA VILE MAGONJWA NA UMASIKINI.
NINAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA KUWA, MIMI KAMA MSANII NINAE ANGALIWA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YA WATU WENGI PANDE MBALI MBALI ZA TANZANIA.
LEO HII NIMEUNGANA NA HOSPITALI YA CCBRT KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.
UAMUZI HUU UMEKUJA BAADA YA CCBRT KUNIALIKA KUTEMBELEA WODI MBALIMBALI ZA WAGONJWA ZILIZOPO HOPITALINI HAPA.
LAKINI BINAFSI NILIGUSWA ZAIDI NA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA FISTULA, UKIZINGATIA PIA MIMI NI MWANAMKE NIKAKUBALI KUUNGANA NA CCBRT ILI KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE WALIO WENGI..
TANGU NIZALIWE MPAKA NAKUWA MKUBWA NA KUFIKIA HATUA NILIOPO HIVI SASA, NAKIRI SIKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA MGONJWA WA FISTULA. MPAKA NILIPOTEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT
NIMESIKITISHWA ZAIDI BAADA YA KUELEZWA KUWA WANAWAKE WENGI WENYE UGONJWA HUU HUSHINDWA KUFANYA KAZI WAKATI MWINGINE HATA KUTENGWA AU KUJITENGA NA JAMII ZAO WANAMOISHI KUTOKANA NA KUWA WANAVUJA HAJA NDOGO AU HAJA KUBWA KILA MARA BILA WAO WENYEWE KUPENDA WALA KUJIJUA. KWAKUWA WANAKUWA WANASHINDWA KUJIZUIA.
HIVYO KUPELEKEA WANAWAKE HAO WENYE FISTULA KUENDELEA KUISHI MAISHA DUNI YA UPWEKE NA KUENDELEA KUWA MASKINI
LABDA NIONGELEE KWA KIFUPI KUHUSIANA NA FISTULA.
NI UGONJWA UNAOWAPATA WASICHANA NA WANAWAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA NA HII HUTOKANA NA KUSHINDWA KUFIKA VITUO VYA AFYA VYENYE HUDUMA YA UZAZI.
FISTULA NI UGONJWA UNAOZUILIKA NA UNATIBIKA.
HAKUNA MWANAMKE ANAETAKIWA KUISHI NA FISTULA HASA UKIZINGATIA CCBRT INATOA MATIBABU, USAIFIRI, CHAKULA NA MALAZI BURE KWA WAGONJWA WOTE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.
JUKUMU LANGU KUBWA KATIKA UBALOZI HUU NI KUSIMAMA NA KUTUMIA SAUTI YANGU, NA NAFASI NILIONAYO KATIKA JAMII KAMA MWANAMUZIKI KUTOA WITO KWA WAGONJWA WENYE FISTULA NA HATA WALE WANAJAMII WENGINE WOTE WANAOFAHAMU WAGONJWA HAO, WAJE CCBRT KUPATA MATIBABU NA HUDUMA ZOTE BURE.
NITAFANYA HAYO POPOTE NITAKAPOPATA NAFASI YA KUONGEA NA JAMII INAYONIZUNGUKA, AMA IWE KATIKA MAONYESHO YANGU AU MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI.
NITAFANYA HIVYO PIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMIII, NINAYOHUSIKA NAYO KAMA BLOGS NA FACEBOOK NA HATA KATIKA MATANGAZO YA TV, RADIO NA VIPEPERUSHI.
ILIMRADI TU UJUMBE UWAFIKIE WANAWAKE WENYE FISTULA WAJE KUTIBIWA BURE CCBRT.
NDUGU ZANGU WAANDISHI WA HABARI, NAOMBA MJIUNGE NAMI KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WENYE FISTULA
ASANTENI SANA
LADY JAYDEE a.k.a KOMANDOO
No comments:
Post a Comment