Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Patrick Tsere akiwa meza kuu na viongozi wa jumuiya ya Watanzania mjini Mzuzu nchini Malawi. Aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa muda Ndugu Ashibon Kinabo.
Katika mkutano huo Mheshimiwa Balozi aliwaeleza umuhimu wa Watanzania hao kuwa na jumuiya yao wenyewe ili kushughulikia kero zao na pia kushirkiana katika masuala yao mbali mbali yanayowahusu wao. Watanzania hao walikubaliana na ushauri aliutoa Balozi Tsere na baada ya hapo walichagua viongozi wao wa muda ambao kazi yao itakuwa pia kuandaa katiba ya jumuiya yao.
Balozi Tsere aliahidi kuwa atazipa kipau mbele katika kushughulikia kero zao zinazowakabili hasa zile za kunyanyaswa na kusumbuliwa na maafisa wa Polisi ya Malawi. Aidha aliwafahamisha wananchi hao kuwa yeye yuko tayari kukutana nao wakati wowote ama kwa wao kufika ubalozini ili kupata huduma, au kwa yeye mwenyewe au maafisa wa ubalozi kufika Mzuzu na kukutana nao kama alivyofanya.
Balozi Partick Tsere wa tatu kutoka kushoto kwenye picha ya pamoja na viongozi. Wa kwanza kushoto ni Bi Mbonile Mwakatundu Katibu wa Kwanza wa Ubalozi anayeshughulikia masuala ya kikonsula.
Balozi Partick Tsere akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waliohudhuria mkutano huo

No comments:
Post a Comment