Sunday, May 30, 2010

Nakaaya na Siasa!

NAKAAYA AJITOSA KUWANIA UBUNGE WA VITI MAALUMU ,MUZIKI APUMZIKA KIDOGO

Nakaaya Sumari akihurubia katika harakati zake za jamii


WAKATI vuguvugu la uchaguzi mkuu likiendelea kushika kasi nchini mwanamuziki wa maarufu wa kizazi kipya nchini,Nakaaya Sumari ameamua kujitosa katika kinyang”anyiro cha kuwania ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama cha demokarisia na maendeleo(Chadema) kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo mjini Arusha.

Nakaaya ambaye ni katibu mhamasishaji wa baraza la vijana wa Chadema wilayani Arusha alichukua fomu ya kuwania kiti hicho juzi katika ofisi za chama hicho zilizopo maneeo ya Esso jengo la Meru Plaza mjini Arusha.

Akiwa ameongozana na mwenyekiti wa vijana wa Chadema wilaya ya Arsuha.Exaud Mamuya sanjari na katibu wa vijana,Arnold Kamnde,mgombea huyo alichukua fomu ya kuwania kiti hicho majira ya saa 3;30 asubuhi katika ofisi hizo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania kiti hicho Nakaaya alisema ya kuwa binafsi anahisi ya kuwa nafasi ya yeye kuwa mwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Arusha katika bunge la jamhuri nchini kupitia chadema mkoani Arusha umewadia.

Nakaaya alisema ya kuwa lengo kubwa lililomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kutokana na uchungu alionao hususani mateso wanayopata wakinamama katika masusla ya afya ya uzazi katika huku akihaidi kusimamia masula ya afya ya uzazi kwa wakianamama nchini.

“nahisi muda umefika wa kutenda ninayoyahubiri siku zote,nataka nikasimamie matatizo ya uzazi kwa wakinamama hili linanipa uchungu katika maisha yangu siku zote”

“nataka nikawawakilishe wnawake wa mkoa wa Arusha kupitia chama changu nina imani nitashinda nafasi hii kwasababu ninajiamini, hivyo naomba mniunge mkono wanawake’alisema Nakaaya

Awali akimkabidhi fomu ya kuwania nafsi hiyo katibu wa Chadema wilayani Arusha,Bakari Kasembe aliwataka wanawake wote wa mkoa wa Arusha kupitia chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hiyo.

Kasembe alisistiza ya kuwa awali chama chao hakikuwa na uwakilishi wa kiti hicho mkoani Arusha katika bunge la jamhuri nchini lakini wakati huu wamejipanga kutoa viti vitatu na kiti cha ubunge wa Arusha mjini.

Tayari joto la kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama hicho limeanza kushika kasi ambapo hadi sasa tayari wagombea wawili wameshajitokeza kuwania kiti hicho ambao ni Magreth Olotu na Joyce Muya.

No comments:

Post a Comment