Monday, May 24, 2010

HATIMAYE LIYUMBA AHUKUMIWA

Matukio wakati wa hukumu ya Liyumba leo
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Benki Kuu Amatus Liyumba akiwa kizimbani dakika chache baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutumua vibaya madaraka wakati wa ujenzi wa maghorofa pacha ya benki hiyo jijini Dar. Mahakimu wawili kati ya watatu walimwona Liyumba ana hatia wakati mmoja alimwona hana hatia. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya wengi wape, hukumu ya miaka 2 inasimama.
Chumba namba moja cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara tu baada ya hukumu kusomwa. Hawa karibu na picha ni mawakili wa serikali

mawakili wa serikali baada ya hukumu kusomwa wakili wa Liyumba Mh. Majura Magfu akiteta na mteja wake baada ya hukumu

Liyumba akishauriana na mawakili wake baada ya hukumu.
Angalizo: habari kamili na video
vinafuata baada ya muda



No comments:

Post a Comment