Wednesday, May 12, 2010

DARAJA LA PAMOJA LAZINDULIWA RASMI LEO.

Maraisi JK na Guebuza wazindua daraja la umoja leo
Daraja la Umoja linavyoonekana kwa juu
Daraja la Umoja kwa pembeni
Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji wakikata utepe kufungua rasmi daraja la Umoja huko Mtambaswala,wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara leo asubuhi Daraja hili linaunganisha nchi hizi mbili na ni kielelezo cha mshikamano na udugu wa kihistoria uliopo baina ya watu wa nchi hizo.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 720 na upana wa meta 13.5 ni kiunganishi kizuri kwa nchi hizi na tunatarajia litatumiwa kwa maslahi ya watu wa Tanzania na Msumbiji, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya barabara. Ni ukombozi kwao.

Wazo hilo lililotolewa na marais waasisi; marehemu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji mwaka 1975 na kutekelezwa na viongozi waliofuata na kukamilishwa na waliopo sasa.

Wazo limesimamiwa na mkandarasi M/s China Geo- Engineering ambaye alisimamiwa na Mhandisi Mshauri NorConsult kutoka Norway, kwa uvumilivu wao na juhudi kubwa za kukamilisha daraja hilo, ambalo litabaki kuwa alama ya uhusiano mzuri na wa kihistoria wa nchi hizi.



No comments:

Post a Comment