Wednesday, May 12, 2010

BROWN AJIUZULU UWAZIRI MKUU.

Cameron awa waziri Mkuu Mpya wa uingereza
Malkia Elizabeth II akisalimiana na Waziri Mkuu
mpya wa Uingereza Bw. David Cameron


Gordon Brown leo amejiuzulu Uwaziri mkuu baada ya chama chake kushindwa kupata viti vya kuweza kuendesha serikali katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi na vile vile amejiuzulu kuwa kiongozi wa chama cha Labour Party.


Chama cha Labour Party kilitakiwa kufikisha viti 326 ili kuweza kuendesha serikali ya nchi lakini hakikuweza kufikia viti hivyo.

Katika uchaguzi huo Labour Party ilipata viti 258, Conservative walipata viti 306, Liberal Democrats walipata viti 57 na vyama vingine walipata kura 28.

Uchaguzi wa mwaka huu umevifanya vyama Conservative na Liberal Democrats kuungana ili kuweza kuchukua madaraka ya kuunda serikali ya kuongoza nchi.

Brown amewasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II endapo Malkia atakubaliana na ombi lake, na anamshauri Malkia kumwita kiongozi wa chama pinzani kuweza kuunda serikali.

Wakati huohuo, David Cameron achaguliwa kuwa Waziri mkuu nchi Uingereza baada ya chama chake kuweza kujiunga na chama cha Liberal Democrats kuunda serikali ya mseto.

Cameron amezaliwa tarehe 9 mwezi wa kumi mwaka 1966 jijini London, amechukua nafasi ya kukiongoza chama cha Conservative tangu mwaka 2005.

Amesomea masomo ya Philosophy, Politics and Economics at Oxford na kupata degree.

Kuchukua madaraka ya kuwa Uwaziri Mkuu kumemfanya Cameron kuwa kiongozi mwenye umri mdogo kuongoza nchi toka mwaka 1812.

No comments:

Post a Comment