Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa maadhimisho ya tamasha la Malaria Duniani lililofanyika kimataifa leo kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar,akisoma hotuba mbele ya wananchi waliofurika kwa wingi wakiwemo wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari.
Wanachi waliofurika viwanjani hapo leo mchana huku jua kali likiwaka wakiadhimisha siku ya Malaria Duniani,huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Kikwete.
Waziri wa Wizara ya Afya Mh. David Mwakyusa akisoma hotuba iliondaliwa kwa ajili ya siku ya maadhimisho ya Malaria Duniani mbele ya Wananchi waliofurika kwa wingi leo mchana katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Msanii ambaye pia ni balozi wa Malaria hapa nchini Prof Jay akiimba nyimbo zake kadhaa jukwaani zilizowavutia wengi uwanjani hapo na kujikuta wakipiga mayowe na shangwe za hapa na pale.

Wasanii ambao pia ni mabalozi wa Malaria hapa nchini, Pichani Marlow na Banana Zorro wakiimba wimbo wa Zinduka malaria haikubaliki kwa kupokezana jukwaani huku umati wa watu ukishangilia.

Umati wa watu waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani wakishangilia,siku hiyo adhimu Kimataifa imefanyika nchini Tanzania jijini Dar katika viwanja vya Mnazi mmoja leo mchana na mgeni rasmi alikuwa ni Rais Jakaya Kikwete.

Mabalozi wa Zinduka Malaria haikubaliki (ambao wote ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya) wakiimba kwa pamoja jukwaani wimbo wao maalum wa Malaria haikubaliki mbele ya umati wa watu katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.

Wasanii kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kufanya igizo lao ufupi lililokuwa limebeba ujumbe mwanana kabisa namna ya kupambana na Mbu aambukizaye malaria.

Meza kuu ya viongozi mbalimbali ikiongozwa na Mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani,ambapo Kimataifa imefanyikia jijini Dar ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Viongozi na watu mbalimbali wakiwa wamesimama kwa pamoja wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari wakiwa wamejumuika kwa pamoja katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani,ambapo Kimataifa imefanyikia jijini Dar ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja na mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.

Pichani kati ni Mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete,Shoto ni Waziri wa Afya ,David Mwakyusa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar,Mh Lukuvi wakiwa wamesimama kwa pamoja wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa mapema leo mchana wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani,ambapo Kimataifa imefanyika jijini dar na kuhudhuriwa na umati wa wa Watu.

Maadhimisho hayo ya siku ya Malaria Duniani ilikuwa ikirushwa hewani na vituo kadhaa vya televisheni na redio,Ikiwemo TBC1 kama uonavyo pichani ikiwe imetega mitambo yake huku wakazi wa majumbani wakiendelea kupata/kufahamu yaliyokuwa yakijiri kwenye viwanja vya Mnazi mmoja leo mchana.

Mitambo ya kituo cha televesheni ya Star TV ambao nao pia walikuwa wakirusha Live matukio mbalimbali ya siku ya Malaria Duniani.

Baadhi ya Washiriki wa siku ya Malaria Duniani wakimsalimia Mkongwe wa muziki wa Taarabu hapa nchini Bi Kidude ambaye pia ni mmoja wa mabalozi wa Malaria Tanzania,shoto ni Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya Mlimani Park Rehan Bichuka ambaye naye ni mmoja wa mabalozi wa Malaria.

Umati wa Watu

Jukwaa la Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani linavyoonekana

Watu kutoka sehemu mbalimbali walipita kwenye geti hili kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Malaria Duniani,ambapo Kimataifa siku hiyo imeazimishwa Tanzania jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa,huku wakiongozwa na Mgeni Rasmi Mh Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment