Sunday, April 25, 2010

GHASIA MPAKANI NA DAFUR ZAUWA ZAIDI YA 50

Ghasia mpakani na Darfur zauwa 55
ramani ya Sudan
Sudan
Kabila moja la huko Darfuri linasema kuwa watu wake 55 wameuawa katika mapigano na askari wa jeshi la Sudan ya kusini.

Msemaji wa kabila la Rezeigat amesema kuwa wachungaji wa mifugo walikuwa wakitafuta malisho ya mifugo mapambano yalipozuka siku ya ijumaa karibu na mpaka wa Sudan ya kusini.

Hata hivyo wakuu wa Sudan ya kusini wamelaumu vikosi kutoka utawala wa kaskazini kwa shambulio hilo. Hata hivyo hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu takwimu za majeruhi.

Ghasia za hivi sasa ndiyo kali kuwahi kutokea tangu uchaguzi wa kihistoria uliofanyika kati ya tareh 11 na 15 mwezi huu.

Matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyochelewa hivi sasa yanatazamiwa kutangazwa siku ya jumatatu kote nchini Sudan.

No comments:

Post a Comment