Sunday, April 25, 2010

MUUNGANO WATIMIZA MIAKA 46

ENZI ZA MWALIMU..................!

http://zanzibardaima.files.wordpress.com/2008/07/muungano-ukoloni.jpg




RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Kitaifa leo Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru.


http://www.mzalendo.net/wp-content/uploads/2009/12/Jakaya-safarini.jpg


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maadhimisho na Sherehe za Taifa, sherehe hizo zitaambatana na gwaride ambalo litapita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, halaiki, sarakasi pamoja na vikundi mbalimbali vya burudani, zikiwemo ngoma za asili.

Kaulimbiu ya siku ya leo ni “Tudumishe Muungano, mhimili wa Taifa Letu.” Tanganyika na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964 kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati huo chini ya waasisi wawili, marais Julius Nyerere na Amani Abeid Karume, ambao kwa sasa wote ni marehemu.

Muungano huo umekuwa mfano kwa nchi mbalimbali duniani kutokana na jinsi Tanzania ilivyoendelea kuudumisha kwa miaka mingi, licha ya changamoto kadhaa zinazoukabili.

Katika siku za karibuni, kumekuwepo na changamoto mbalimbali za Muungano zikiwemo za mgawanyo wa rasilimali baina ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.

Hivi karibuni, Wazanzibari wamekuwa wakitaka suala la mafuta ambalo ni sehemu ya mambo ya Muungano libaki kwao na lisiwe suala la muungano huo; jambo ambalo limezua mjadala mzito, huku serikali ikieleza kuwa linaweza kuondolewa tu endapo theluthi mbili ya wabunge wataridhia.

No comments:

Post a Comment