Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh .William Lukuvi akizungumza na wafanyakazi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani akishiriki kuimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) .
Wafanyakazi kutoka Mashirika na Taasisi mbalimbali na vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) wakiwa kwenye maadamano kuelekea viwanja vya Mnazi mmoja kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani inayoadhimishwa leo kitaifa jijini Dar es salaam.
Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya mnazi mmoja
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki za NBC, NMB pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) wakiwa wameshikana mikono huku wakiimba wimbo wa “ MSHIKAMANO DAIMA” leo katika viwanja vya Mnazi mmoja kuadhimisha siku ya Kazi Duniani.
Wasanii wa Muziki wa Dansi kutoka katika kundi la Akudo Impact (Vijana wa Masauti) wakitoa burudani leo katika viwanja vya Mnazi mmoja katika maadhimisho ya siku ya Kazi Duniani.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa wameungana na wafanyakazi kuadhimisha siku ya kazi Duniani iliyofanyika kitaifa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Baadhi ya vijana waliohudhuria sherehe hizo wakicheza kwa furaha ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja kuunga mkono maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanayoadhimishwa leo kitaifa jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment