Maelfu ya abiria wa safari za ndege waliokuwa wamekwama barani Ulaya wanatarajiwa kuanza safari hivi karibuni, wiki moja baada ya wingu la majivu yaliyotokana na mripuko wa volkano nchini Iceland kusababisha usumbufu wa safari hizo.
Viwanja vya ndege vya Ujerumani vilifunguliwa tena hapo jana na kuruhusu ndege 5,000 kuingia na kutoka nchini humo. Idadi hiyo ni karibu theluthi mbili ya safari za kawaida.
Shirika kubwa la ndege la Ujerumani, Lufthansa lilitangaza kuwa safari zake zote za ndege zitaendelea hii leo kama kawaida. Zaidi ya safari 95,000 za ndege zilifutwa na sasa litakuwa jukumu la mashirika ya ndege kukabiliana na matatizo yaliyotokana na kufutwa kwa safari hizo.
No comments:
Post a Comment