Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imezitolea mwito nchi 27 wanachama wa umoja huo kutekeleza ahadi zao walizotoa kwa ajili ya misaada ya maendeleo.
Mwaka uliopita nchi za Umoja wa Ulaya zilitoa jumla ya Euro bilioni 49 kwa ajili ya mataifa masikini, ambazo ni sawa na asilimia 0.42 ya pato la ndani la taifa.
Juhudi zaidi zinahitajika kwa Umoja wa Ulaya kufikia malengo ya asilimia 0.56 ya pato la ndani la taifa kwa mwaka huu.
Kiasi hicho kiliahidiwa kama sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
No comments:
Post a Comment