Wednesday, April 21, 2010









https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7tIVmao_QZAIU1ejJpdLp5qLkUwtXEQb9akmicckaM9v7xkRgELOgu8p9UTrF8sM5pOcL3g4LILDSBf32ZHHWWJp5LDMf2fSxjjTQVDpYa526YT3YqohEmTPaVpRKfFBOL8QR0Po7aGKj/s320/Matumla1.jpg



BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini Rashid Matumla amesema kuwa yupo tayari kuzichapa na mshindi wa pambano kati ya Maneno Oswald (Mtambo wa Gongo) na Mada Maugo ambalo linatarajia kufanyika Jumamosi Aprili 24 katika ukumbi wa DDC Kariakoo.

Jana Matumla alisema kuwa anatamani Maugo Aweze kushinda pambano hilo la jumamosi ili aweze kupambana naye na kumuonyesha kuwa ujuzi hauzeeki.

"Natamani sana kupambana na Maugo kwa sababu nyingi tu huku kubwa zaidi ikiwa ni kutaka kumuonyesha kuwa ujuzi hauzeeki,"alisema Matumla.

"Niko tayari wakati wowote ule ili kuhakikisha nailinda na kuiendeleza heshima ya mabondia wakongwe hapa nchini," alisema Matumla.

Mbali na hilo amemtahazarisha Maneno Oswald kuwa makini zaidi katika pambano hilo kwani Maugo amejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha analipa kisasi kufuatia kutandikwa katika pambano la kwanza ambalo
liliwakutanisha mabondia hao

No comments:

Post a Comment