Monday, October 4, 2010

HATIMAYE MTANDAO WA SIMU UNAOONGOZA TANZANIA WATIMIZA MIAKA KUMI!


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania kwa kutoa huduma ya miaka kumi nchini Tanzania.hafla hii imefanyika asubuhi ya leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akitoa ufafanuzi katika mkutano na waandishi wa habari juu ya mtandao wa Vodacom utakavyoboreshwa baada ya kutoa huduma zake kwa muda wa miaka kumi hapa nchini.Mkurugenzi wa uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akikaribisha maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari waliofikam leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski wakati wa mkutano wa Vodacom kusherehekea miaka kumi kwa kutoa huduma zake hapa nchini.
Baadhi ya wakurugenzi wa Vodacom Tanzania wakijibu maswali mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Dietlof Mare wa tatu kutoka kushoto.
Baadhi ya wakurugenzi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika sherehe ya Vodacom kutimiza miaka kumi ya kutoa huduma zake hapa nchini.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Vodacom wakiangalia picha mbalimbali tangia Vodacom ilipoanzishwa hapa nchini.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto)akipozi kwa picha na Mkurugenzi wa Mauzo Exaud Kiwali.
Kutoka kushoto Mtaalamu wa Mambo ya Habari wa Vodacom Matina Nkurlu,Meneja Mawasiliano wa Vodacom Nector Foya,Afisa Habari wa Vodacom Kilasa Mtambalike,wakiwa wamepozi kwa picha mara baada ya sherehe ya miaka kumi ya Vodacom Tanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wakiangalia historia fupi ya Vodacom Tanzania tangia ianze kutoa huduma zake hapa nchini.
Baadhi ya wakurugenzi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment