Ni furaha na tabasamu ya kutosha kabisa kutoka kwa binti Geneviev Emanuel pichani kutoka kitongoji cha Temeke,ambaye ndiye aliyelinyakua taji la Miss Tanzania 2010 usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,Mwenge jijini Dar na kuhudhuriwa na watu kibao.
Mshindi wa taji la Miss Tanzania 2010 Geneviev Emanuel ambaye ameibuka na kulinyakua taji hilo adhimu kwa kuwapiku walimbwende 30 kutoka vitongoji mbalimbali.Pichani Miss Tanzania 2010 Geneviev Emanuel akikabidhiwa rasmi usiku wa kuamkia leo gari yake aina ya Hyundai i10 lenye thamani ya shilingi milioni 12 pamoja na kitita cha shilingi Millioni 10.
No comments:
Post a Comment