Rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua (pichani) amefariki mapema leo katika Ikulu ya nchi hiyo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Serikali imetangazaa siku saba za maombolezo na kubainisha kwamba Rais huyo atazikwa siku ya Alhamisi ijayo.
Makama wa Rais Goodluck Jonathan aliyekuwa Kaimu Rais tokea mwezi wa Februari, anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo yenye watu wengi barani Afrika.
Marehemu Yar'Adua, 58, alishika madaraka toka mwaka 2007 akiahidi mabadiliko mengi, na wachunguzi wa mambo wanasema alifanya makubwa katika kuleta amani kwenye eneo tajiri la mafuta la bonde la Niger.
Mungu ailaze roho ya marehemu Yar'Adua mahala pema peponi Amen!
Mungu ailaze roho ya marehemu Yar'Adua mahala pema peponi Amen!
No comments:
Post a Comment