
KATIKA mechi ya fainali ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Afrika Kusini Julai 12, siyo tu kombe maarufu la dunia ambalo litakuwa linang'ara kwenye Uwanja wa Soccer City kwa sababu kampuni ya Adidas imeonyesha mpira rasmi utakaotumika kwenye mechi ya fainali ambao una rangi ya dhahabu unaoitwa JO'BULANI ambao umetokana na mipira ya JABULANI ambayo ni rasmi kwa mechi nyingine za fainali hizo kuanzia Juni 11.
Jina la JO'BULANI limetolewa kwa heshima ya jiji la Johannesburg ambalo linafahamika pia kama "City Gold"(Jiji la dhahabu) au Jo'burg, ambapo mipira hiyo JO'BULANI bado haina tofauti kubwa sana na mipira ya JABULANI ambayo ilibuniwa Afrika Kusini,lakini langi kubwa ya mipira ya JO'Bulani ni dhahabu.
Hii ni mara ya pili kampuni ya adidas inabuni mipira rasmi kwa ajili ya mechi ya fainali ya kombe la dunia. Mpira wa kwanza wa fainali kubuniwa na adidas uliitwa TEAMGEIST BERLIN ambao ulitumika katika fainali iliyochezwa Julai 9,2006. Mipira ya JO'BULANI imeanza kuuzwa rejareja jana na itaendelea kuuzwa.
Mipira ya JABULANI na JO'BULANI yote ni ubunifu mpya, ambapo inatarajiwa itawavutia wachezaji kwa sababu haipei na ipo katika umbo sahihi la duara.
Jina JO'BULANI limetokana na jina JABULANI ambalo maana yake ni tusherekee kwa lugha ya isiZulu ambayo ni lugha mojawapo kati ya lugha rasmi 11 zinazozungumzwa nchini Afrika Kusini, isiZulu inazungumzwa na asilimia 25 ya raia wa Afrika Kusini. Pia jina JO'BULANI limetolewa kwa heshima kwa jiji ambalo linaandaa mechi ya fainali ya kombe la dunia Johannesburg au Jo’burg kama linavyoitwa na wengi.
Mpira wa JO'BULANI umebuniwa kwa rangi nyeupe na dhahabu kwa heshima ya kombe la dunia ambalo lina rangi ya dhahabu na jiji la Johannesburg"City of Gold"(Jiji la dhahabu). |
No comments:
Post a Comment