Treni iendayo kasi barani Afrika, imeanza safari yake mpya kuelekea mji mkuu, Pretoria, kutoka Johannesburg katika jitahada za kurahisisha usafiri baina ya miji hiyo mikubwa ya Afrika Kusini.
Treni hiyo ijulikanayo kwa Gautrain inachukua chini ya dakika thelathini kwa safari ya umbali huo wa kilometa 54.
Kwa gari mwendo wa safari hiyo huchukua hadi saa mbili wakati watu wengi wakiwa wanatumia usafiri kwenda ama kurejea kazini.
Safari ya treni hiyo ya Gautrain kwa njia ya kueleka uwanja wa ndege ilizinduliwa wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, ambapo maelfu ya mashabiki wa soka waliitumia kusafiria.
Lakini kwa kufika Pretoria, inaonekana itatumia zaidi na wasafiri wa kawaida nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na foleni katika barabara yenye magari mengi nchini humo.
Mamia ya watu walimiminika katika kituo cha treni cha Rosebank mjini Johannedburg tangu mapema saa kumi na moja na nusu alfajiri kuwahi treni ya kwanza iliyoelekea Pretoria.
Kulikuwa na matatizo kidogo yalijitokeza, ikiwemo matatizo ya kiufundi katika behewa moja, lakini wahandisi wamesharekebisha tatizo hilo, kwa mujibu wa maafisa wa Gautrain.
Serikali imesema lengo lake ni kuufanya usafiri wa treni ndio uti wa mgongo wa mfumo wa usafiri wa umma, kwa mujibu wa Waziri wa Usafiri, Sbu Ndebele.
Treni hiyo ya Gautrain imegharimu randi bilioni 24 sawa na dola bilioni 3 kuijenga.
Kasi ya treni hiyo ni kilometa 160 kwa saa.
Gautrain inatarajiwa kupunguza idadi ya magari katika barabara ya N1 Ben Schoeman inayounganisha Pretoria na mji wa kibiashara wa Afrika Kusini wa Johannesburg kwa asilimia 20.
No comments:
Post a Comment