Thursday, September 23, 2010

WANAHABARI WANOLEWA NA PCCB MKOANI MOROGORO

wanahabari wanolewa na PCCB mkoani morogoro
Mkuu wa dawati la Elimu ya Umma wa PCCB Mkoa wa Morogoro, Mercy Manyalika ( wa kwanza kulia) akitoa mada iliyohusu ufahamu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi , pamoja na ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010, kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) Septemba 21, mwaka huu mjini hapa ( wapili kutoka kustoto ) ni Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro, Stela Mpanju na ( wa kwanza (kushoto) ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro , Ahamed Msangi kutoka Jeshi la Polisi, ambaye ni Mwenyekiti wa Dawati la uchaguzi Mkoa Mkoa kama mwalikwa.
Mwanasheria wa PCCB Mkoa wa Morogoro, Debora Mlowe ( wa kwanza kulia) akifafanua jambo kuhusu sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi , inayoendana na ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) Septemba 21, mwaka huu ambayo iliandaliwa mahusisi na Taasisi hiyo kwa waandishi wa habari wa Mkoani Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Polisi , wakishiriki mafunzo ya siku moja ya kuzifahamu sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi ,pamopja na ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu mjini hapa.Picha na John Nditi.

No comments:

Post a Comment