Saturday, April 17, 2010

Waangalizi waukosoa uchaguzi Sudan


Wakaguzi wa uchaguzi













Mashirika mawili ya kimataifa yanayofanya uangalizi wa uchaguzi nchini Sudan yamesema upigaji kura haukufikia viwango kamili vya kimataifa.

Muungano wa Ulaya na kituo cha rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, wamesema kulikuwa na dosari kubwa, wakitaja kutishwa na kusumbuliwa kwa wapiga kura.

Hata hivyo mashirika hayo yamesema uchaguzi huo ni hatua kubwa ya kuelekea katika demokrasia.

Matokeo yanatazamiwa kuanza kutolewa siku ya Jumanne, huku Omar al-Bashir akitazamiwa kupata ushindi wa urais.

Uchaguzi huo, wa rais, wabunge na wa tawala za mikoa, ni wa kwanza chini ya vyama vingi tangu mwaka 1986, na ni sehemu ya mpango wa amani kati kaskazini na kusini, wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miongo miwili.

No comments:

Post a Comment